Viongozi wa mashirikisho ya soka barani Afrika, wamekubaliana kwa kauli moja kumuunga mkono Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kwa muhula wa tatu mwaka ujao.
Viongozi wa CAF wakiongozwa na Rais Patrice Motsep,e waliafikia haya baada ya kukutana pembezoni mwa kongamano la 76, la FIFA, jijini Vancounver,Canada.
CAF inamuunga mkono Infantino, kuchaguliwa kwa muhula wa tatu kati ya mwaka 2027 na 2031.
Kongamano 77 la uchaguzi wa CAF, litaandaliwa nchini Morocco mwaka ujao.