Wanariadha zaidi ya 17,000 wamejiandikisha kushiriki makala ya tano ya mbio za Nairobi Marathon zitakazoandaliwa Jumapili hii.
Kati ya idadi hiyo, wanariadha 1,750 watashiriki mbio za kilomita 42 huku wengine 5,050 wakitimka nusu marathon.
Mbio za kilomita 10 zimewavutia washiriki 6,550 wakati zile za kilomita 5 zikiwa na wanariadha 4,100.
Barabara kadhaa za kuingia na kutoka jijini Nairobi zitafungwa kuanzia usiku wa manane Jumamosi hadi Jumapili saa nane.
Washindi wa mbio za kilomita 42 watatutzwa shilingi milioni 3.5, nafasi ya pili milioni 2.25 na nambari tatu milioni 1.5