CAF yaanza ukaguzi wa viwanja vya CHAN nchini Uganda,Kenya na Tanzania

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeanza ukaguzi wa viwanja vitakavyotumika kuandaa fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani yaani CHAN mwaka ujao.

Kinyang’anyiro hicho kitaandaliwa katika mataifa ya Afrika mashariki ;Kenya,Uganda na Tanzania kati ya Februari mosi na 24 mwakani.

Ujumbe wa CAF unaowajumuisha wataalam kutoka idara mbalimbali wanafanya ukaguzi huo kati ya Novemba 22 na 30 mwaka huu ,kutathmini hali ya maandalizi.

Ujumbe huo pia utakagua miundo mbinu kama vile mikahawa,viwanja vya ndege na maeneo ya kufanyia mazoezi, ili kuhakikisha wameafiki viwango vinavyohitajika.

Huu ni ukaguzi wa pili wa CAF katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki ,baada ya ule wa kwanza wa Septemba 17 na ukafuatiwa na ziara ya Rais wa CAF Patrice Motsepe.
27 na 30 .

Ujumbe wa CAF umekuwa Kampala, Uganda kati ya tarehe 21 hadi 24 Novemba,ikifuatwa na Dar es Salaam kuanzia tarehe 4 hadi 27, na hatimaye Nairobi,Kenya baina ya tarehe

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article