Simba wakabiliwa na mtihani mkubwa dhidi ya Berkane

Mchuano huo utang'oa nanga  saa nne usiku katika uwanja wa Municipal de Berkane.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka Tanzania bara klabu ya Simba, watashuka dimbani kumenyana na RS Berkane ya Morocco, katika duru ya kwanza ya fainali kuwania kombe  la shirikisho la soka Afrika.

Mchuano huo utang’oa nanga  saa nne usiku katika uwanja wa Municipal de Berkane.

Pambano la maruidio litasakatwa katika uwanja wa Amaani kisiwani Zanzibar Mei 25.

Simba wanacheza fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza miaka miwili tangu Yanga washindwe pia fainalini na klabu ya US Alger ya algeria.

Website |  + posts
Share This Article