CAF 2025: Kenya Police yafungwa pingu na Zamalek ya Misri

Tom Mathinji
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa kombe la mashirikisho barani Afrika CAF, Zamalek ya Misri, wamefuzu katika awamu ya makundi baada ya kuishinda Kenya Police ya Kenya jumla ya mabao 3-1.

Mabao mawili yaliyofungwa na Ahmed ‘Zizo’ Sayed na Nasser Maher, ziliihakikishia nafasi katika awamu ya makundi, huku Jesse Were akifunga bao la kufuta machozi, katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa kimataifa wa Cairo.

Timu ya Kenya Police, sasa imebanduliwa katika michuano hiyo ya Kombe la Mashirikisho Barani Afrika, CAF.

Baada ya kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza bao moja kwa bila juma lililopita uwanjani Nyayo hapa jijini Nairobi, wawakilishi hao wa Kenya walifanya mashambulizi makali katika mechi ya marudiano jijini Kairo, lakini juhudi zao hazikufua dafu.

Wakati huo huo, mabingwa wa Ligi Kuu ya soka ya humu nchini Gor Mahia, watamenyana na Al-Ahly ya Misri, katika mechi ya marudiano ya awamu ya mwanzo ya ligi ya kilabu bingwa Barani Afrika, jijini Kairo, Misri leo jioni.

Aidha, timu ya Gor Mahia itakosa huduma za kipa chaguo la kwanza Kevin Otieno, anayeuguza jeraha.

Share This Article