Bunge la taifa lapongeza uamuzi wa Mahakama ya Upeo kuhusu ushiriki wa umma

Tom Mathinji
2 Min Read
Kikao cha bunge la taifa.

Bunge la taifa limepongeza uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Upeo uliofafanua ushiriki wa umma katika mchakato wa kisheria.

Uamuzi huo uliotolewa Oktoba 29,2024, ulidokeza kuwa ushirikishaji wa umma katika mswada wa fedha wa mwaka 2023, ulitimiza viwango vinayohitajika kikatiba.

Katika uamuzi uliotolewa na jopo la majaji saba, lililoongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome, Mahakama hiyo ya upeo iliamua kuwa ushiriki wa umma katika mswada wa fedha wa mwaka 2023 ulitekelezwa kikatiba.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu haki na maswla ya sheria Gitonga Murugara, ambaye ni mbunge wa Tharaka, akipongezqa uamuzi huo alisema,”Tunapongeza mahaka aya upeo kwa kufafanua kuhusu jisni ushiriki wa umma unavyopaswa kutekelezwa.”

Akiunga mkono matamshi hayo, kiongozi wa wengi katika bunge la taifa aliyepia mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wa, alisema kuwa ushiriki wa umma mara nyingi haujaeleweka na nyakati nyingine kutafsiriwa visivyo na mahakama.

“Mahakama ya upeo imetoa mwongozo na msingi dhabiti kwa majaji na watungaji sheria kuhusu ushiriki wa umma,” alisema mbunge huyo.

Kiongozi wa wachache katika bunge hilo Junet Mohamed wa Suna Mashariki alisema kuwa,” Jambop la muhimu ambalo Mahakama ya Upeo imefafanua ni jukumu la bunge kutoa habari kwa umma, uamuzi huo unaimarisha uwezo wetu wa kisheria kwa niaba ya wakenya.”

Naye mbunge wa Molo Kimani Kuria alipendekeza kuwa kabla ya kushirikisha umma katika mswada wowote wa fedha, ni vyema umma kuelimishwa kwanza.

Naibu mwenyekiti wa kamati ya haki na maswala ya katiba Mwengi Mutuse wa Kaitialisema mahakama hiyo ya upeo imetoa mwongozo bora kuhusu kutekelezwa kwa ushiriki wa umma.

Share This Article