Billnass ampamba Nandy kwa maneno anapoadhimisha siku ya kuzaliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Tanzania William Nicholaus Lyimo maarufu kama Billnass amemmiminia mke wake Nandy ambaye pia ni mwanamuziki maneno matamu anapoadhimisha siku ya kuzaliwa.

Baba huyo wa mtoto mmoja alichapisha picha yao ya harusi na picha nyingine za awali kuashiria safari yao ya mapenzi na kuandika “Ninapaswa kumshukuru Mungu, kwa kunipa mke na rafiki ndani ya nafsi moja, ninakupenda sana mke wangu Hata dunia ingeanza upya kesho bado ningetafuta Nafasi ya kukuoa!!”

Mwanamuziki huyo aliendelea kusema kwamba Nandy hufanya azidi kumpenda huku akimtakia heri njema kwenye siku yake ya kuzaliwa.

“Nina mengi ya kusimulia ulimwengu Kuhusu upendo wangu kwako…ila kwa leo acha niseme Beki zangu kwako hazikabi kabisa…nakupenda mpaka nakupenda tena ❤️ Happy Birthday” alimalizia mwimbaji huyo ambaye kwa sasa anahudumia marufuku ya BASATA.

Nandy alijibu ujumbe huo akisema, “Nakupenda MUME WANGU sana sana sana sana MUNGU atutunze.”

Binti huo alizaliwa Novemna 9, 1992.

Nandy na Billnass walifunga ndoa Jumamosi Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT huko Mbezi Beach Dar es salaam na wamejaliwa mtoto mmoja wa kike.

Share This Article