Bidhaa za Kenya zapigwa marufuku kuingia Sudan

Martin Mwanje
1 Min Read
Wajumbe wa RSF wakiwa Nairobi mwezi Februari mwaka huu

Sudan imetangaza kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa kutoka Kenya. 

Mwezi jana, Kenya ilikuwa mwenyeji wa wajumbe wa Kundi lenye Hadhi ya Kijeshi la (RSF) la Sudan katika hatua ambayo imeighadhibisha Khartoum.

Taarifa ya kupigwa marufuku uagizaji wa bidhaa kutoka Kenya ilitangazwa na Kaimu Waziri wa Bishara wa Sudan, Omar Ahmed Mohamed Ali.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uagizaji wa bidhaa zote kutoka Kenya kupitia bandari, viwanja vya ndege, mpakani na vituo vya kuingia nchini Sudan umesitishwa kuanzia jana Alhamisi hadi hatua hiyo itakapobatilishwa.

Wakiwa jijini Nairobi tarehe 22 mwezi Februari mwaka huu, wajumbe wa kikosi cha RSF na washirika wake wa kisiasa na makundi yenye silaha walitia saini “mkataba wa kisiasa” na kuelezea nia ya kuunda “serikali mbadala” nchini Sudan.

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *