Mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa katika jiji kuu la Uganda,Kampala, na viunga vyake imesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara baada ya kuharibu bidhaa za mamilioni ya pesa.
Maji ya mafuriko yamezagaa ndani ya maduka ya kufanyia biashara jijini Kampala, yakiwemo maduka ya kuuza nguo ,mikahawa na maeneo ya burudani na kuharibu mali.
Yamkini mafuriko hayo yamesababishwa na mfumo mbovu wa upitashaji maji taka jijini Kampala.
Wafanyabiashara karibu na kituo kikuu cha mabasi jijini Kampala cha Qualicel, wamehansgaishwa pakubwa na mafuriko hayo waking’ang’ana kuzoa maji ndali ya maduka yao ili waendelee na bishara zao.
Aidha,wasafiri wa magari,pikipiki na hata watembea miguu wamelazimika aidha, kuogelea au kupita ndani ya maji ya mafuriko hali inayohatarisha maisha yao.