Benki ya Equity yanakili faida ya Shilingi Bilioni 48.8

Tom Mathinji
1 Min Read
Benki ya Equity yanakili faida ya shilingi bilioni 48.8.

Benki ya Equity imetangaza faida ya shilingi bilioni 48.8, katika Kipindi kilichokamilika Mwezi Disemba mwaka 2024.

Faida hiyo ilinakiliwa katika kile kilichotajwa na benki hiyo kuwa riba ya juu ya mikopo.

Kulingana na ripoti ya benki hiyo, mapato jumla ya riba yaliongezeka kwa asilimia 9.3 hadi shilingi bilioni 170.3, huku mapato yasiyokuwa na riba yakiongezeka kwa asilimia 10.7 hadi shilingi bilioni 85.1.

Wakati wa Kipindi hicho benki hiyo ilipunguza utoaji mikopo kwa wateja wake kwa asilimia 8 na kunakili shilingi bilioni 819.2 ikilinganishwa na shilingi bilioni 887.4 mwaka 2023.

Afisa Mkuu mtendaji wa benki hiyo Dkt. James Mwangi alisema anatarajia kuwa utoaji wa mikopo wa benki hiyo kwa wateja utaongezeka kwa kati ya asilimia 10 hadi 15.

“Tuna matumaini kwamba utoaji mikopo mwaka huu utaongezeka kwa kati ya asilimia 10 na 15,” alisema Mwangi.

Hata hivyo gharama za operesheni ziliongezeka hadi shilingi bilioni 133.04 katika kipindi hicho kilichokamilika mwezi Disemba mwaka 2024.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *