Mwanablogu akamatwa kwa kuchapisha habari za kupotosha

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanablogu akamatwa kwa kuchapisha habari za uwongo.

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), wamemkamata mwanablogu kwa madai ya kuchapisha habari za kupotosha kwenye ukurasa wake wa TikTok.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa X, DCI ilisema Roy Otieno Odhiambo alitiwa nguvuni baada ya kupachika video kwenye ukurasa wa TikTok iliyodai alilipwa shilingi milioni 3.5 ili amuue mtu mashuhuri hapa nchini.

Kulingana na DCI, video hiyo ilipachikwa Oktoba 20, 2025.

“Kufuatia uchunguzi dhidi ya madai hayo, maafisa hao wa upelelezi walimkamata Odhiambo kutoka maficho yake mjini Malindi,” ilisema DCI.

DCI imesema mshukiwa huyo sasa anasubiri kufikishwa mahakani.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article