Murkomen: Maafisa wa uokoaji wametumwa Elgeyo Marakwet

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Waziri wa Usalama wa  Taifa Kipchumba Murkomen, ametuma risala za rambirambi kwa wakazi wa wadi za Endo, Sambirir, na Embobut, kaunti ndogo ya Marakwet Mashariki, kaunti ya Elgeyo Marakwet, kufuatia maafa na uharibifu wa mali uliosababishwa na maporomoko ya ardhi.

Akituma rambirambi hizo leo Jumamosi kupitia ukurasa wa X, waziri huyo alisema serikali imetuma helikopta za polisi na jeshi zikiwa na waokoaji na wahudumu wa afya, ili kushrikiana na maafisa wa Shirika la Msalaba mwekundu katika shughuli inayoemndelea ya uokoaji.

“Tunashirikiana na serikali ya kaunti ya hii na washirika wengine wasio wa serikali ili kushughulikia janga hilo pamoja na kutoa usaidizi kwa familia zilizoathiriwa,” alisema Murkomen.

Juhudi za kukarabati barabara zilizoharibiwa na maporomoko hayo ya ardhi zinaendelea, kufanikisha uchukuzi wa dharura na wa kutoa misaada.

Watu kumi wamethibitishwa kufariki huku wengine wengi wakiripotiwa kutoweka kufuatia maporomoko hayo makubwa ya ardhi yaliyotokea kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Website |  + posts
Share This Article