Benki kuu ya Libya imetangaza kwamba imesitisha huduma zake zote na kwamba hazitarejelewa hadi pale ambapo afisa mmoja mkuu wa benki hiyo aliyetekwa nyara atakapoachiliwa huru.
Benki hiyo ambayo makao yake makuu yako jijini Tripoli ndiyo ya pekee inayotambuliwa kimataifa na ndiyo hutumika kupokea malipo ya mafuta yanayouzwa nje.
Mafuta ndiyo namna ya kipekee ya serikali pinzani za Libyamoja yenye makao yake makuu huko Bengazi na nyingine jijini Tripoli, kujipatia mapato.
Kulingana na benki hiyo mtu asiyejulikana anahusika na utekaji nyara wa Musaab Muslam, anayesimamia idara ya teknolojia ya mawasiliano kwenye benki hiyo siku ya Jumapili.
Katika taarifa usimamizi wa benki kuu ya Libya ulisema kwamba haitakubali njia zisizo halali ambazo watu wengine wanatumia.
Taarifa hiyo ilielezea pia kwamba maafisa wengine wa benki hiyo walitishiwa na hivyo huduma zinasitishwa hadi yanayoendelea yakomeshwe na maafisa wa usalama wachukue hatua.
Balozi wa Marekani nchini Libya Richard Norland, alisema wiki jana kwamba majaribio ya kubadilisha usimamizi wa benki kuu kwa lazima yangefanya nchi hiyo iondolewe kwenye soko la kimataifa la fulusi.
Norland alifanya mkutano na gavana wa benki hiyo kuu Sadiq Kabir kujadili vitisho kutokakwa makundi yaliyojihami ambayo yalikuwa yanakusanyika nje ya benki hiyo jijini Tripoli.
Kulingana na balozi huyo, suala la ugavi wa mapato ya Libya ni lazima litatuliwe kwa njia wazi na majadiliano jumuishiili kuafikia bajeti inayokubalika na wote.
Libya ilifurahikia amani kiasi tangu maandamano ya mwaka 2011 yaliyoungwa mkono na NATO na ambayo yalisababisha kuondolewa mamlakani kwa kiongozi wa kiimla Muammar Gaddafi.
Iligawanyika tena mwaka 2014 kati ya makundi kinzani ya mashariki na magharibi mwa nchi hiyo.