Baraza la Sanaa la Taifa – BASATA ambalo linahusika na udhibiti wa tasnia ya sanaa na burudani nchini Tanzania, limetangaza usajili wa mameneja wa wasanii na waandaaji wa matukio.
Katika taarifa ya Aprili 8, 2025, Katibu Mtendaji wa BASATA Kedmon Mapana kwamba wahusika wote wanafaa kuwa wamejisajili na BASATA kufikia Aprili 30, 2025.
Kulingana na BASATA hatua hiyo inalenga kuhakikisha kwamba shughuli zote za sanaa na matukio zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ya serikali.
Kanuni za BASATA zinaelekeza kwamba mameneja wa wasanii, wapiga muziki yaani DJs na asanii wenyewe wasajiliwe ili kupata kibali cha kufanya kazi hizo.
Baraza hilo linatumai pia kuwezeshwa kufuatilia na Kusimamia shughuli za sanaa kwa uwazi na ufanisi zaidi, kupitia usajili huo.
Usajili huo unaweza kufanywa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti BASATA ambayo anwani yake ni www.basata.go.tz.