Azimio yamtaka Rais Ruto kusaini mswada wa kuunda upya IEBC

Dismas Otuke
1 Min Read
Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.

Muungano wa Azimio One Kenya umemtaka Rais William Ruto kuidhinisha mswada wa kuunda upya kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC.

Katika mkutano na wanahabari, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema ni hatari kubwa kwa nchi kukosa kuwa na tume hiyo, hali ambayo imechangia maeneo mengine ya bunge na uwakilishi wadi kukosa wawakilishi.

Kalonzo pia amemtaka Rais Ruto kuitisha uchaguzi kutokana na maandamano yanayoendelea kote nchini yakiongozwa na kundi la vijana wa Gen Z.

Ameishutumu serikali kwa kile alichokidai kuwa ilikodisha magenge ya majambazi yaliyopora mali wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *