Awamu ya pili ya uuzaji tiketi za AFCON yafunguliwa huku tiketi 230,000 zikiuzwa katika awamu ya kwanza

Dismas Otuke
1 Min Read

Kamati andalizi ya Makala ya 35 ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), nchini Morocco, imetangaza kuwa jumla ya tiketi 230,000 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza kutoka nchi 74 kote duniani.

Idadi ya tiketi zilizo uzwa katika awamu ya kwanza zinajumuisha asilimia 40 ya tiketi zote za kipute hicho kitakachoandaliwa Moroko kati ya Disemba 21 mwaka huu na Januari 18 mwaka ujao.

Tiketi zote zinazohusisha wenyeji katika mechi za makundi tayari zimemalizika.

Asimilia 30 ya tiketi zitauzwa katika awamu ya pili kupitia kwa APP ya FAN ID.

Website |  + posts
Share This Article