Arsenal walianza kutetea taji hya Ligi Kuu Uingereza vyema baada ya kuwalabua Coventry City mabao 3-0, Ijumaa uisku uwanjani Emirates.
Kai Havertz alifungua ukurasa kwa bao la dakika 15 kabla ya Bukayo Saka, kutanua uongozi dakika 7 baadaye na kwenda mapumzikoni kwa uongozi wa 2-0.
Kipindi cha pili The Gunners waliendeleza na makali yao huku nahodha Martin Odegard akipachika la tatu dakika ya 49.
Mechi nyingine za kufungua msimu Jumamosi, Hull City watawaalika Manchester United, Everton wakwangurane na Crystal Palace, Ipswich wakabane koo na Sunderland, Leeds United iwatembelee Nottingham Forest wakati Brentford wakifunga ratiba dhidi ya Tottenham katika Derby ya London.
Jumapili, Aston Villa watakutana na Brighton, Manchester City wawe nyumbani kupimana nguvu na Bournemouth, kisha Liverpool wafunge wikendi dhidi ya Newcastle United.
Fulham watakamilisha raundi ya kwanza kwa kuwaalika Chelsea Jumatatu usiku.