Wanyonyi awika Laussane Diamond League

Wanyonyi alitumia muda wa dakika 1 sekunde 42.19, kuvuka mstari wa mwisho na kudumisha uongozi wake msimu huu ambapo sasa amezoa pointi 35.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 800 Emmanuel Wanyonyi, alijituma kibabe kabla ya kushinda mkondo wa 12 wa Diamond League mjini Laussane Uswizi.

Wanyonyi alitumia muda wa dakika 1 sekunde 42.19, kuvuka mstari wa mwisho na kudumisha uongozi wake msimu huu ambapo sasa amezoa pointi 35.

Djamel Sedjati wa Algeria alimaliza wa pili kwa dakika 1 sekunde 42.31,huku Miller Brandon wa Marekani, akimaliza wa tatu.

Bingwa wa Olimpiki Faith Cherotich, alimaliza wa pili katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji akitumia dakika 9 sekunde 1.90,nyuma ya Winfred Yavi aliyeibuka mshindi kwa dakika 9 na nukta 4,akifuatwa na Marwa Bouyazani wa Tunisia.

Bingwa wa Dunia katika mita 800 Lillian Odira, aliambulia nafasi ya saba huku Audrey Werro wa Uswizi akiibuka mshindi,akifuatwa na Femke Bol wa Uholanzi naye Saida Tsehaye wa Ethiopia akamaliza wa tatu.

Share This Article