Annie Idibia katika hatari ya kukatwa mguu

Jeraha kwenye mguu wake linasemekana kuanza kuoza na madaktari wanapendekeza mguu ukatwe.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwigizaji Annie Idibia wa Nigeria anaripotiwa kuwa katika hatari ya kukatwa mguu kufuatia jeraha ambalo limekataa kupona tangu alipolipata mwaka jana.

Kulingana na jukwaa la mitandaoni la habari la Gistlover, hali ya Annie inazidi kuwa mbaya kutokana na kile kinachosemekana kuwa uraibu uliokithiri wa pombe na dawa za kulevya.

Inaripotiwa kwamba mguu wake unaoza katika sehemu ambapo jeraha hilo lipo na sasa madaktari wanapendekeza kwamba mguu huo ukatwe ili kumnusuru.

Familia yake inaripotiwa pia kutafakari kumpeleka India kwa matibabu zaidi ambapo wanatumai watapata pendekezo mbadala kutoka kwa madaktari.

Mke huyo wa mwanamuziki 2Face Idibia au 2Baba anaripotiwa kutaka kumwona mumewe hospitalini alikolazwa kufuatia msongo wa mawazo uliotokana na hatua ya 2Face ya kutangaza kwamba wametengana na wanaendeleza taratibu za talaka.

Umma ulikisia kwamba Annie ana tatizo la uraibu wa pombe na mihadarati kufuatia tabia yake kwenye kipindi cha Netflix kiitwacho ‘Young, Famous and African’ ambapo mara nyingi yeye huzungumza kama mlevi.

Uraibu huo umesababisha mabadiliko makubwa katika hulka yake kiasi cha yeye kutojali afya yake kama kupona kwa jeraha hilo.

Kakake kwa jina Wisdom wakati mmoja alijitokeza kwa umma na kumlaumu kwa kumwonyesha jinsi ya kutumia dawa za kulevya lakini baadaye akakanusha usemi wake akitaja msongo wa mawazo.

Haya yanajiri wakati ambapo 2Baba anaripotiwa kumchumbia mpenzi wake wa sasa aitwaye Natasha.

Mamake 2Baba naye alitoa wito hivi maajuzi wa maombi na usaidizi wa maafisa wa usalama katika kuokoa mwanawe kwani anaamini Natasha anatumia ushirikina kumshika 2Baba.

Mama huyo anasema 2Baba alihepa kutoka nyumbani kwao na hawajui aliko lakini wanaamini amefichwa na Natasha.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *