Ahly kumenyana na Esperance katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Watetezi wa taji ya Ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly ya Misri waliwazidia maarifa washindi mara tano Toupiza Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ,mabao matatu kwa bila Ijumaa usiku katika duru ya pili ya nusu fainali.

Mkumbo wa kwanza ulikuwa umemealizikia sare tasa mjini Lubumbashi.

Ahly watakuwa wakicheza fainali kwa mara ya nne katika muda wa miaka mitano huku wakiwania taji ya 12 kwa jumla.

Katika marudio mengine ya semi fainali mjini Pretoria wenyeji Mamelodi Sundowns, walibanwa goli moja kwa sifuri na mabingwa mara nne Esperance kutoka Tunisia.

Espernace walifuzu kwa fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli mawili kwa bila na watakumbana na Ahly katika mkondo wa kwanza Mei 19 huku marudio yakipigwa Cairo Mei 26.

Mabingwa watatuzwa dola milioni 1.5 za Marekani na kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Saudi Arabia.

Share This Article