Afueni kwa waathiriwa wa maporomoko ya ardhi Tinderet

Marion Bosire
1 Min Read
Gavana Sang akipanda mti Tinderet

Zaidi ya wakulima 500 walioathirika na maporomoko ya ardhi Katika eneo la Tinderet kaunti ya Nandi wana kila sababu ya kutabasamu Baada ya kuchimbiwa mitaro ya kupitisha maji.

Wamepatiwa pia miche ya kahawa na nyasi na serikali ya Kaunti ili kuboresha ukulima na kuzuia mmomonyoko wa udongo ambao umekuwa ukishuhudiwa kila mara.

Lukas Simatwo wa umri wa Miaka 96 ni mmoja wa wakulima wa kijiji cha Kaplamaiywo ambao wamekuwa wakipitia changamoto si haba kutokana na hasara walizopata baada ya mazao yao na mchanga kusombwa na maji kila wakati kufuatia maporomoko ya ardhi wakati wa mvua kubwa.

Aidha wakulima hao wamedokeza kwamba eneo hilo la Tinderet ni moja kati ya maeneo yaliyotengwa kimaendeleo nchini ambapo umaskini umekithiri lakini kupitia mpango huo sasa wataweza kuzalisha chakula chao na kujipatia mapato mazuri mbali na kulinda mazingira.

Gavana wa Kaunti ya Nandi Stephen Sang amewataka wakulima hao wakukumbatie kilimo cha kahawa na upanzi wa nyasi katika maeneo yanayoporomoka ili kusaidia kushikilia mchanga na kuwawezesha kufanya kilimo bila matatizo yoyote.

Wakulima hao wasiojiweza walipewa Miche 200 ya Kahawa Kila moja wakati wa uzinduzi wa mpango huo wa SNL ambao unalenga kuwachimbia mitaro ya Kilomita 40 ili kuimarisha kilimo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *