Achani: Serikali ya Kwale inaimarisha utoaji huduma bora za afya

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Kwale Fatuma Achani afungua Zahanati ya Bonje, Kaunti ya Kwale.

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani, amesema serikali yake inajizatiti kuhakikisha wakazi wa kaunti hiyo wanapata huduma zilizoimarika za afya.

Achani alisema hayo yanaafikiwa kupitia ujenzi wa vituo vipya vya afya, utoaji wa vifaa vya matibabu katika vituo vya afya na kuhakikisha vituo hivyo, vina wafanyakazi wa kutosha.

“Ni jukumu letu kama serikali kuhakikisha vituo vyetu vya afya vina vifaa vya kutosha na vinafanyakazi kiikamilifu,” alisema Achani.

Aliyasema hayo alipofungua zahanati ya Bonje katika eneo la Mwamdudu kaunti ndogo ya Kinango.

Kulingana na Achani, zahanati hiyo inapaswa kuwahudumia wakazi 3,000 katika maeneo ya Chongongwe, Mwangoka, Zagwaru na Bonje.

Hadi kufikia sasa, Achani alisema serikali ya kaunti ya Kilifi, imejenga vituo 178 vya afya na kuwaajiri wahudumu 1,800 wa afya.

Waliohudhuria afya hiyo ni pamoja na waziri wa afya wa kaunti hiyo, Francis Gwama, maafisa wakuu wa afya Dkt. Kitsao Mjimba na  Athman Mwashando miongoni mwa wengine.

Share This Article