Achani agawa vifaa kazi kwa wanafunzi waliohitimu Kwale

KBC Digital
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani ameongoza shughli za ugavi wa vifaa vya kazi kwa wanafunzi 42 waliohitimu kwenye mafunzo tofauti tofauti kutoka vyuo mbalimbali vya kiufundi katika kaunti hiyo.

Vifaa hivyo vikiwemo vifaa vya mapishi, ususi, mashine za kunyolea, tarakilishi, vifaa vya kutengezea magari pamoja na vya umeme, vimetokana na juhudi za serikali ya kaunti ya Kwale kupitia mradi wa KEMSFED unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Hadi kufikia sasa, serikali ya kaunti hiyo imejenga na kuweka vifaa vya kisasa katika vyuo 43 vya kiufundi pamoja na kuajiri zaidi ya walimu 130 wa vyuo hivyo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo katika makao makuu mjini Kwale, Achani amewahimiza vijana kujiunga na vyuo vya kiufundi ndani ya kaunti hiyo ili kujipatia mafunzo yatakayowasaidia kubuni nafasi za ajira na kujiendeleza kimaisha.

KBC Digital
+ posts
TAGGED:
Share This Article