KCB watawazwa mabingwa wa ligi ya Voliboli baada ya miaka 15

Marion Bosire
1 Min Read

Waliokuwa mabingwa wa Afrika katika Voliboli ya Afrika katika Voliboili ya Waanwake ,klabu ya Kenya Commercial Bank, imetwaa taji ya ligi kuu, baada ya kustahimili ukinzani mkali na kuwashinda waliokuwa mabingwa wa mwaka jana Kenya Pipeline seti 3-1, katika fainali ya mchujo wa kitaifa uwanjani Nyayo siku ya Jumatano.

Pipeline walianza kwa makeke wakishinda seti ya kwanza alama 25-18 ,lakini wahifadhi hela wakageuza na kuwatofya katika seti tatu zilizofuatia kwa alama 25-19, 25-21 na 25-21.

Magereza wamemaliza nafasi ya tatu baada ya kuwalemea timu ya DCI seti 3-1 za 25-21, 19-25, 25-16 na 25-21.

Share This Article