Watu 14 wamefariki kwenye mashua ya wahamiaji Uhispania

Watu sita walipelekwa hospitali kwa helikopta wakiwa katika hali mbaya.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 14 wamepatikana wamefariki kwenye mashua ya wahamiaji Uhispania

Wahamiaji 14 wamethibitishwa wameaga dunia, baada ya mashua iliyokuwa na takriban watu 100 kuokolewa karibu na Visiwa vya Canary, Uhispania, hayo ni kulingana na Waziri wa Kimaeneo Angel Victor Torres.

Mashua hiyo iliyookolewa baada ya kuwa baharini kwa siku kadhaa, ilipatikana kilomita 72 kusini mwa kisiwa cha El Hierro siku ya Ijumaa.

Kulingana na huduma za uokoaji wa majini ya Uhispania, watu sita walipelekwa hospitali kwa helikopta wakiwa katika hali mbaya.

“Imethibitishwa kuwa wahamiaji 14 walifariki kwenye mashua iliyowasili El Hierro,” alisema Torres.

Visiwa vya Canary vimekumbwa na ongezeko kubwa la wahamiaji, likifikia rekodi ya watu 2,100 kwa siku moja mnamo Novemba 25, wengi wakielekea El Hierro.

Mkasa huu umetokea siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Uhispania, ambapo suala la uhamiaji ni mojawapo ya hoja kuu za kampeni.

Share This Article