Mwanamume katika kaunti ya Busia, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kupatikana na vifaa vinavyohusiana na ugaidi, na kukusanya taarifa kwa lengo la kuwezesha shughuli za kigaidi.
Hakimu Mkuu wa Busia Nyaloti Ameyo, alimpata Allan Odhiambo, almaarufu Isaa Odhiambo hatia kwa mashtaka mawili chini ya sheria ya kuzuia ugaidi.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimwondolea mashtaka ya kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi.
Upande wa mashtaka ulifahamisha mahakama kwamba Odhiambo akiwa mwenye ufahamu alimiliki simu ya rununu iliyokuwa na video zaidi ya 80 zenye uhusiano na makundi ya kigaidi ya Al-Shabaab na ISIS, zilizotoa mafunzo ya kigaidi, mauaji na kueneza propaganda zenye itikadi kali.
The prosecution presented forensic, electronic and expert evidence in support of the case.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kisayansi, kielektroniki na kiutaalam katika kupiga jeki kesi hiyo.
Odhiambo ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya mashtaka dhidi yake na hukumu aliyopewa.