King Saha azungumza baada ya madai ya Winnie wa Mummy

Alidai kwamba Saha alikuwa akimpiga mara kwa mara, hali iliyomlazimu kuondoka kwenye uhusiano huo, kutafuta amani na maisha bora.

Marion Bosire
1 Min Read
King Saha

Mwanamuziki wa Uganda King Saha, amekanusha madai mazito ya unyanyasaji wa kimwili yaliyotolewa na aliyekuwa mpenzi wake, Winnie Wa Mummy.

Winnie alitoa madai hayo wakati wa mazungumzo mubashara kwenye TikTok ambapo alieleza kwamba uhusiano wake na mwanamuziki huyo ulijawa maumivu.

Alidai kwamba Saha alikuwa akimpiga mara kwa mara, hali iliyomlazimu kuondoka kwenye uhusiano huo, kutafuta amani na maisha bora.

Kwa mujibu wa Winnie, madai hayo ya kunyanyaswa yalimwacha na majeraha ya kisaikolojia na hofu ya mara kwa mara kuhusu usalama wa maisha yake.

Alidai kuwa hata wanafamilia na marafiki hawakujua alikokuwa amejificha wakati akijaribu kurejesha utulivu wa maisha yake.

Kufuatia madai hayo, King Saha aliingia kwenye mitandao yake ya kijamii na kuchapisha jumbe tata zilizotafsiriwa kuwa huenda zilikuwa majibu yake kuhusu sakata hilo, ingawa hakuyazungumzia madai hayo moja kwa moja.

“Ukimya ni rafiki wa kweli ambaye huwa hasaliti kamwe. Mungu amlinde na kumpa kila kitu anachostahili.” Aliandika.

Inasubiriwa kuona iwapo King Saha atatoa maelezo zaidi kuhusu yaliyojiri.

Share This Article