Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, ametuma rambirambi kwa serikali na watu wa Afrika Kusini, kufuatia kifo cha Naibu Rais wa zamani Phumzile Mlambo-Ngcuka.
Kwenye ujumbe wake, Uhuru alimkumbuka Naibu huyo wa Rais wa zamani kama kiongozi shupavu, ambaye huduma zake kwa wananchi wa Afrika Kusini, zilichangia kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
Rais huyo mstaafu alimuomba Mungu kuipa familia ya Mlambo-Ngcuka na wananchi wa Afrika Kusini nguvu, faraja na ujasiri wakati huu mgumu wa majonzi.
Mlambo-Ngcuka, alihudumu wadhifa wa Naibu Rais kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008, alipochukua wadhifa wa Jacob Zuma aliyetimuliwa kufuatia madai ya kushiriki ufisadi.