Mudavadi: Masoko na barabara ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi

Mudavadi alikariri umuhimu wa maendeleo endelevu, ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi  maendeleo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Musalia Mudavadi - Mkuu wa Mawaziri.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, amesema masoko ya kisasa na barabara, ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, kupiga jeki biashara ndogo na kubuni fursa kwa jamii.

Akizungumza katika kaunti ya Bungoma, Mudavadi alisema soko la kisasa la Sirisia litakalogharimu shilingi milioni 127, litawanufaisha pakubwa wafanyabiashara wadogo, kwa kutoa mazingira ya ubora wa juu ya biashara.

Kulingana na Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, barabara mpya ya Musikoma–Buyufu–Mungatsi, itafanikisha uchukuzi wa bidhaa hadi sokoni, huduma muhimu na kuimarisha shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

“Miradi hii inabuni sehemu ya mpango mpana wa maendeleo ya kitaifa, inayojumuisha ujenzi wa barabara, uunganishaji umeme, masoko ya kisasa, upanuzi wa reli ya kisasa na miundombinu ya mipakani,” alisema Mudavadi.

Alikariri umuhimu wa maendeleo endelevu, ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi  maendeleo.

Mudavadi alikuwa ameandamana na Rais William Ruto kwa ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya maendeleo katika kaunti ya Bungoma.

Rais Ruto yuko kwenye ziara ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa nchi.

Share This Article