Tanzania kupata katiba mpya kufikia mwaka 2029

Kulingana na Rais huyo, kwa sasa tume ya maridhiano inabuniwa ambayo itajukumiwa na kuunda katiba mpya.

Tom Mathinji
1 Min Read
Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema taifa hilo litapata katiba mpya kufikia mwaka 2029.

Kulingana na Rais huyo, kwa sasa tume ya maridhiano inabuniwa ambayo itajukumiwa na kuunda katiba mpya.

Rais huyo alisema serikali tume hiyo ya maridhiano ya kitaifa, ambayo inatatangazwa hivi karibuni, itaimarisha umoja wa taifa na kuweka msingi wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini.

Aidha, alidokeza kuwa serikali yake imeanza mashauriano na makundi mbalimbali, yakiwemo viongozi wa dini, vyama vya siasa na taasisi za kiraia, ili kupata wawakilishi watakaoshiriki katika tume ya maridhiano.

Kiongoozi huyo wa taifa, alisema usalama wa nchi hiyo sasa ni dhabiti baada ya kuyumbishwa na msukosuko wa tarehe 29 Oktoba mwaka 2025.

“Kama mnavyojua tulikumbwa na msukosuko mwaka wa 2025, ila hali ya usalama nchini imeimarika.Kutokana na hayo tuliunda tume kuchunguza yaliyotokea,na tayari tumeanza kutekeleza mapendekezo ya tume hiyo.
Kinachofuata sasa ni kuunda tume ya maridhiano kuelekea uundaji wa katiba” alisema Rais Suluhu.

Share This Article