Watu wanne wafariki baada ya mashua kuzama Nigeria

Mashua hiyo inayodaiwa ilikuwa na abiria kupita kiasi, ilipinduka baada ya kukumbwa na hitilafu za kiufundi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu wanne wafariki baada ya mashua kupinduka nchini Nigeria.

Watu wanne wamethibitishwa kufariki, baada  ya mashua iliyokuwa imewabeba mamia ya waombolezaji kupinduka kusini mwa Nigeria.

Kulingana na msemaji wa polisi Musa Mohammed, mashua hiyo inayodaiwa ilikuwa na abiria kupita kiasi, ilipinduka baada ya kukumbwa na hitilafu za kiufundi, ilipokuwa ikisafiri kutoka Ayama kuelekea Ukubie.

Alisema waliofariki walijumuisha watoto wawili na watu wazima wawili.

Hata hivyo, Mohammed alidokeza kuwa watu 24 waliokolea, 19 wakitibiwa katika kituo kimoja cha afya katika eneo hilo na watato walipelekwa katika hospitali kwenye mji mkuu wa jimbo hilo.

Makundi ya uokoaji yanaendelea kuwatafuta waathiriwa.

Dereva wa mashua hiyo anadaiwa kutoroka, lakini polisi wamesema msimamizi wa mashua hiyo anazuiliwa korokoroni.

Share This Article