Msanii mkongwe wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Besta aliyewahi kutamba na nyimbo za Baby Boy na Kati Yetu, amesema yeye na Mume wake, Msanii Marlaw, wanaendelea kuishi vizuri.
Akizungumza kwenye mahojiano, msanii huyo alifafanua kwamba ndoa yao haina changamoto na wanashirikiana kulea Watoto wao wanne.
Besta amesimulia safari yake ya muziki aliyoianza akiwa na umri mdogo, akieleza mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa muziki.
Anasema mapenzi hayo ya muziki yalisababisha adanganye Wazazi wake ili wampatie fedha za kurekodi wimbo na video, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kutimiza ndoto ya kuwa Msanii.
Marlaw alitamba miaka ya awali kwa nyimbo kama “Binti Kiziwi”, “bembeleza” na “Pii Pii” kabla ya kuingia kipindi cha kimya kirefu kimuziki.
Alipenda sana kuimba kanisani akiwa na umri mdogo kabla ya kuingilia muziki kama taaluma. Jukwaa la kwanza kubwa alipata ni mashindano ya uimbaji ya Coca-Cola Popstars, mwaka 2004.
Mafanikio yake katika tasnia ya muziki yalionekana sana kati ya mwaka 2007 na 2010.
Wimbo wake maarufu wa “Pii Pii” ulishinda tuzo ya TMA yaani Tanzania Music Awards mwaka 2010, katika kitengo cha wimbo bora wa mtindo wa Afro Pop.
Wanandoa hao wawili wanashiriki tamasha ya mzunguko ya miaka 30 ya Bongo Fleva.