Mwanamuziki wa Uganda, Cindy Sanyu, ametangaza mipango ya kuandaa tamasha kubwa mwaka ujao, huku Lugogo Cricket Oval ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa onyesho hilo la Machi 12, 2027.
Tamasha hiyo iliyopatiwa jina la “The Woman King”, inaashiria hatua nyingine muhimu katika safari ya muziki ya Cindy, anapojiandaa kuwapa mashabiki wake burudani ya aina yake.
Mwimbaji huyo alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo alishiriki video iliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba, ikionyesha dhana ya mwanamke mfalme na kuwapa mashabiki taswira ya ujumbe na mandhari ya tamasha hiyo.
Tangazo hilo pia linaashiria mabadiliko ya eneo la kufanyia tamasha kwa Cindy, ambaye mwaka jana aliandaa onyesho lake la ‘The Royal Experience’ ndani ya Lugogo Millennium Park.
Safari hii, amechagua Lugogo Cricket Oval, ambayo ina nafasi kubwa zaidi ya kuhudumia mashabiki.
Akiwa na zaidi ya miaka kumi katika tasnia ya muziki na akijulikana kwa maonyesho yenye mvuto, Cindy anatarajia kufanya ‘The Woman King’ kuwa moja ya matukio makubwa katika kalenda ya burudani nchini Uganda.
Anajiunga na orodha ya wasanii wa Uganda ambao tayari wameanza kupanga matamasha makubwa mwaka 2027.
Miongoni mwao ni Kataleya na Kandle, ambao pia wametangaza mipango ya kufanya tamasha, ingawa bado hawajafichua tarehe wala eneo litakalotumika.