Kenya ndiyo mwenyeji wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa wabunge kuhusu njaa na utapiamlo.
Rais William Ruto anaufungua mkutano huo rasmi leo Jumatatu, Novemba 16, 2026, katika majengo ya Bunge jijini Nairobi.
Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha wabunge zaidi ya 250 na wadau wa maendeleo kutoka mabunge mbalimbali duniani kujadili mikakati ya kukabiliana na njaa na utapiamlo.
Huu ni mwaka wa kwanza kwa mkutano huo wa kimataifa kufanyika barani Afrika.
Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, amekuwa akisimamia maandalizi ya mwisho ya mkutano huo kwa kushirikiana na wabunge, wasimamizi wa Bunge na wafanyakazi wengine.
Mkutano huo unaandaliwa kwa pamoja na Bunge la Kenya, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO na Shirika la Uhispania la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, AECID.
Washiriki wanatarajiwa kujadili hatua za kisheria, kibajeti na kiusimamizi zitakazosaidia kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, kuboresha lishe na kuhakikisha wananchi wanapata haki ya chakula kupitia maendeleo jumuishi na mifumo endelevu ya kilimo.
Majadiliano yataangazia pia changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na kuyumba kwa uchumi.
Mkutano wa Nairobi unajengwa juu ya mikutano iliyotangulia ya Madrid, Uhispania, mwaka 2018 na Valparaíso, Chile, mwaka 2023.