Wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma waongeza nauli

Tom Mathinji
1 Min Read
Wahudumu wa Matatu waongeza nauli.

Wananchi wanatarajiwa kulipa nauli zaidi baada ya wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma, kutangaza kuongeza nauli, saa chache baada ya Halmashauri ya kudhibiti Nishati na Petroli kuongeza bei za mafuta hapa nchini.

Chama cha wahudumu wa matatu nchini kimesema kuwa nauli hizo mpya zitaanza kutekelezwa Aprili 15, 2026.

Mwenyekiti wa chama hicho Albert Karakacha, alisema mabadiliko hayo yalichochewa na kuongezeka kwa bei za mafuta hapa nchini, kulikosababisha kupanga kwa gharama ya operesheni za matatu kote nchini.

“Tunaongeza nauli kutokana na kuongezeka kwa bei za mafuta. Bei za mafuta zimepanda na kuwa vigumu kudumisha nauli ya sasa iliyoko,” alisema Karakacha.

Katika bei mpya za mafuta zilizotangazwa na EPRA, lita moja ya Petroli imeongezeka kwa shilingi 28.69, Dizeli kwa shilingi 40.30, huku bei ya mafuta taa ikikosa kubadilika.

TAGGED:
Share This Article