Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, amemfungulia mashtaka Inspekta wa Polisi Kenneth Kipkemboi Sang, kuhusiana na mauaji ya wakili kyalo Mbobu.
Hatua inafikisha sita, idadi ya walioshtakiwa kuhusiana na mauaji ya wakili huyo aliyeuawa Septemba 9, 2025.
Sang alifikishwa kwenye mahakama ya Kibera siku ya Alhamisi, ambapo alikanusha mashtaka hayo ya mauaji.
Mahakama hiyo iliagiza kuwa Inspekta huyo wa polisi azuiliwe rumande akisubiri kusikilizwa na kuamuliwa iwapo ataachiliwa kwa bondi.
Wengine ambao wameshtakiwa kuhusiana na mauaji hayo ni pamoja na Rose Mbithe Mulwa, Chris Mulwa, Angela Mulwa, konstebo wa polisi Julius Kipkoech Cheruiyot na konstebo wa polisi Kennedy Kipkemboi Borboroi.
Awali walikuwa wamefunguliwa mashtaka kwenye Mahakama Kuu ya Kibera, lakini walikanusha mashtaka hayo.
Upande wa mashtaka utawasilisha ushahidi mahakamani kuthibitisha mashtaka hayo.