Mwanajeshi wa Marekani akamatwa kwa madai ya kuwa jasusi wa Urusi

Alikamatwa siku ya Jumanne karibu na mji wa Gloucester, takriban mita 100 Magharibi mwa London.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanajeshi wa America akamatwa kwa madai ya kuwa jasusi wa Urusi.

Mwanajeshi wa Marekani amekamatwa nchini Uingereza kwa madai ya kuwa jasusi wa Urusi.

Hayo yametangazwa na maafisa wa Marekani na Uingereza.

Jina la afisa huyo mwenye umri wa miaka 41 limebanwa, lakini maafisa wa Marekani wamesema ni afisa wa ngazi za juu katika kambi ya kijeshi ya Imjin.

Alikamatwa siku ya Jumanne karibu na mji wa Gloucester, takriban mita 100 Magharibi mwa London.

Mwanajeshi huyo anashtumiwa kukiuka sehemu ya kwanza na ya tatu ya sheria za usalama za Uingereza za mwaka 2023, kupokea na kusambaza habari zilizolindwa na kutoa usaidizi kwa shirika la kijasusi la kigeni.

Kulingana na Jenerali anayesimamia kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha jeshi la Marekani, mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi jijini London.

“Madai hayo yana uzito na uchunguzi wetu unaendelea,” alisema mshirikishi mkuu wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha Uingereza Vicki Evans kupitia kwa taarifa.

Share This Article