Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wanawake saba upande ilipoteza tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya msururu wa dunia divisheni ya tatu, baada ya kulemewa na Uganda katika nusu fainali ya mashindano ya Afrika.
Kenya Lionesses wakicheza nyumbani katika uwnaja wa RFUEA kaunti ya Nairobi ilipoteza nusu fainali alama 19-14.
Tunisia pia ilifuzu kwa fainali kufuatia ushindi wa pointi 22-10 dhidi ya Zimbabwe katika nusu fainali ya pili.
Matokeo hayo yana maana kuwa Kenya watakosa kushiriki mashindano ya msururu wa Dunia Divisheni ya tatu mwaka ujao.