Meli tatu za mafuta zimeteketezwa mapema Jumapili katika mlango bahari wa Hormuz huku vita kati ya Marekani na Iran vikichacha.
Inaaminika kuwa meli hizo zilikuwa baharini bila kibali ndiposa zikalipuliwa.
Maafisa wa usalama nchini Iran wa kundi la Revolutionary Guard, wamesema meli hizo zimelipuliwa na kuteketea katika eneo la Strait of Hormuz.
Aidha, wanaanga wa Saudi Arabia walidungua mabomu matatu yaliyolipuliwa na kundi la waasi waHouthi kutoka Yeman, na kusababisha kuporomoka kwa jumba la orofa moja mjini Riyadh.
Kundi la Houthi limesa angaa watu 72 waliuawa kwenye mashambulizi ya angani katika mikoa minane ndani ya saa 48.