Rais William Ruto aliwapokea mabingwa wa ligi kuu mara 22 Gor Mahia siku ya Jumapili katika Ikulu ya Nairobi.
Rais aliwapa changamoto Gor Mahia kufanya vyema na kutwaa Kombe la Ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao baada ya kushinda ligi Kuu msimu uliokamilika.
Aidha, Ruto aliahidi kukamilishwa kwa viwanja 28 ifikiapo mwaka ujao vitakavyochangia katika ukuzaji vipaji nchini.
Rais alituza kila mchezaji na afisa wa benchi ya kiufundi shilingi laki moja, huku akitoa kiwango kingine cha shilingi milioni 10 kusaidia maandalizi ya Gor kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.