Rais William Ruto ameondoka nchini Jumapili jioni kuelekea Ulaya kwa ziara rasmi katika mataifa ya Ubelgiji, Norway na Finland.
Kulingana na taarifa ya Ikulu, Rais anatarajiwa kutumia ziara hiyo kushawishi mataifa hayo kuwekeza humu nchini na kupanua masoko ya bidhaa za Kenya ughaibuni.
Kwenye ziara yake nchini Ubelgiji, Rais anatarajiwa kukutana na Mfalme Philipe katika mazungumzo yanayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Ubelgiji.
Aidha, Ruto anatarajiwa kukutana na uongozi wa Umoja wa Ulaya, EU akiwemo Rais wa Baraza la EU António Costa na Rais wa bunge la Ulaya Roberta Metsola.