Vipusa wa Uganda watwaa ubingwa wa raga ya Afrika

Mashindano hayo ya siku mbili yaliyoandaliwa Nairobi, yalileta pamoja timu 11 bora za raga ya wanawake saba upande barani Afrika.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uganda ndio mabingwa wa raga ya Afrika kwa wanawake saba upande  baada ya kuwacharaza Tunisia alama 33-0, katika fainali iliyoandaliwa katika uwanja wa RFUEA kaunti ya Nairobi Jumapili.

Uganda sasa itawakilisha Afrika katika mashindano ya msururu wa dunia  HSBC divisheni ya tatu mwaka ujao.

Mashindano hayo ya siku mbili yaliyoandaliwa Nairobi, yalileta pamoja timu 11 bora za raga ya wanawake saba upande barani Afrika.

Hata hivyo ilikuw apigo kwa wenyeji Kenya ambao wataandaa msururu mmoja wa divisheni ya tatu mwaka ujao katika uwanja wa Raila Odinga.

 

 

Share This Article