M-Pesa yanakili faida ya shilingi bilioni 100 katika nusu ya mwaka

Kwa jumla M-Pesa ilifanya miamala ya kima cha shilingi bilioni 27.4, katika kipindi hicho ikiwa ongezeko la asilimia 25.2.

Dismas Otuke
1 Min Read

Huduma ya M-Pesa ya kutuma na kupokea pesa kupitia kwa simu inayomilikiwa na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, imenakili faida ya shilingi bilioni laki moja katika nusu ya kwanza ya mwaka kwa mara ya kwanza .

Katika kipindi hicho cha miezi sita, Safaricom ilikuwa na ongezeko la asilimia 35.9 ya pato lake ikiwa shilingi bilioni 58.2, kufikia Septemba mwaka huu.

M-Pesa ilizalisha ongezeko la pato lake kwa asilimia 11.3 kufikia shilingi bilioni 226.1, huku pato lake la kabla ya ushuru likiongezeka kwa asilimia 27.5 na kufikia shilingi bilioni 129.2.

Kwa jumla M-Pesa ilifanya miamala ya kima cha shilingi bilioni 27.4, katika kipindi hicho ikiwa ongezeko la asilimia 25.2.

Share This Article