Mradi wa bomba la gesi wa Africa-Atlantic wapiga hatua muhimu

Mwafaka huo ulisainiwa pembezoni mwa mkutano wa mataifa wanachama wa jumuiya uchumi wa Afrika Magharibi EWCOWAS.Mwafaka huo ulisainiwa pembezoni mwa mkutano wa mataifa wanachama wa jumuiya uchumi wa Afrika Magharibi EWCOWAS.

Dismas Otuke
2 Min Read

Mradi wa bomba la gesi wa Africa-Atlantic ulifikia hatua muhimu Julai 19, kufuatia makubaliano kati ya serikali za Morocco na Nigeria mjini Freetown,Sierra Leone.

Mradi huo ulizinduliwa ,mwaka 2016, kufuatia kutiwa saini na Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita na marehemu Rais wa wa Nigeria Muhammadu Buhari,alipozuru Kasri ya Morocco na ingawa ulikuwa haujaanza kutekelezwa rasmi.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, amekariria kuhakikisha kukamilishwa kwa mradi huo kupitia afisi ya kitaifa ya Hydrocarbons and National Petroleum Company Limited (NNPC Ltd.)

Mfalme Mohammed wa 6 wa Morocco,amekuwa akiufuatilia mradi huo ambao ni mojawapo wa ruwaza zake kwa karibu ili, kuhakikisha unatoa suluhisho la changamoto za kawi barani Afrika.

Mwafaka huo ulisainiwa pembezoni mwa mkutano wa mataifa wanachama wa jumuiya uchumi wa Afrika Magharibi EWCOWAS.

Morocco sio mwanachama wa ECOWAS ,ila ilijumuishwa kwenye mkutano huo kutoka kwa wafadhili.

Hatua muhimu itakayofuatia ni kusaini kwa mkabata huo nchini Morocco, ambao utawezesha kutolewa kwa pesa za ujenzi ,mkutano utaongozwa na Mfalme wa 6 na  kuhudhuriwa na Marais Tinubu, na Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania .

Hatua hii inaashiria ushirikiano mwema na wa karibu kati ya Morocco na Nigeria ambao si ushirikiano tu katika sekta ya kawi,bali pia ushirkiano wa kiuchumi,kisiasa na masuala ya kiusalama.

Mradi wa Africa-Atlantic Gas Pipeline punde utakapokamilika utapanua ukuaji wa viwanda,kubuni ajira ,utoshelevu wa kawi barani Afrika na kufungua fursa mpya kati ya Afrika na Ulaya kupitia bahari ya Atlantic.

Share This Article