Wakurugenzi na wasimamizi wa Bodi ya Hakimiliki Kenya, KECOBO wameaga mwenyekiti anayeondoka, Joshua Kutuny, katika hafla ya ghafla iliyofanyika Naivasha.
Hafla hiyo ilihitimisha kikao cha siku mbili cha bodi na usimamizi kilicholenga kupitia na kuidhinisha sera na mikakati ya kuboresha utoaji huduma na kuimarisha sekta ya hakimiliki nchini.
Katika hafla hiyo, wakurugenzi na wafanyakazi walimsifu Kutuny kwa uongozi wake, kujali maslahi ya wafanyakazi na juhudi za kuboresha maisha ya wabunifu katika kipindi chake cha uongozi.
Mkurugenzi Agatha Alutalala alimtaka Kutuny kama kiongozi mwadilifu na mwenye nia njema, huku Dan Aceda akimpongeza kwa kuimarisha umoja, kuzipa kamati za bodi mamlaka zaidi na kuhimiza maamuzi shirikishi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu George Nyakweba pia alisifu upatikanaji wa Kutuny kwa kuwapa ushauri na kujitolea kwake kutetea maslahi ya wabunifu na wafanyakazi.
Kutuny aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa KECOBO Oktoba 2023.
Miongoni mwa mafanikio yake ni kuimarisha usimamizi wa Mashirika ya Usimamizi wa Haki za Pamoja, CMOs, huku mashirika yasiyozingatia masharti yakinyimwa leseni.
Katika kipindi chake, KECOBO pia ilitekeleza ushuru wa vifaa vya kurekodia na kunakili maudhui.
Bodi imesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha wabunifu wanapokea asilimia 70 ya mirabaha inayokusanywa na kunufaika ipasavyo kutokana na kazi zao za ubunifu.