Ruto azuru kaunti za Nandi na Uasin Gishu

Akiwa mjini Kapsabet Rais  pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa na mafunzo kwa gharama ya shilingi nusu bilioni.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumapili ameendeleza ziara yake ya kimaendeleo katika kaunti za Uasin Gishu na Nandi.

Akiwa kaunti ya Nandi Ruto alifungua jumba la  kanisa la Kianglikana nchini (ACK) mjini Kapsabet na baadaye kuhudhuria ibada katika kanisa hilo.

Aidha,alifungua  makao makuu ya kaunti ya Nandi mjini Kapsabet na kukagua ujenzi wa uwanja wa Kapsabet utakaomudu watu 10,000.

Akiwa mjini Kapsabet Rais  pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa na mafunzo ya Kapsabet kwa gharama ya shilingi nusu bilioni.

Rais pia amezindua mradi wa uunganishaji umeme wa last mile wa shilingi milioni 351 katika eneo bunge la Emgwen kaunti ya Nandi ambao utanufaisha nyumba  3,851 kwa stima.

Share This Article