Tusker kumenyana na Singida kwa tiketi ya makundi kombe la Shirikisho

Dismas Otuke
1 Min Read

Tusker FC ya Kenya watashuka uwanjani Airtel Singida, Jumapili usiku kwa mechi ya kufa kupona dhidi ya wenyeji Singida Black Stars ,ikiwa marudio ya mchujo wa pili kuwania kombe la Shirikisho.

Singida walioshinda mkumbo wa kwanza goli moja bila jibu katika uwanja wa Nyayo wiki jana, wanahitaji sare ya  aina yoyote kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Tusker nao watakuwa na mlima wa kukwea wakihitaji ushindi wa 2-1, ili kuingia hatua ya makundi.

 

Share This Article