Salmin Kasimu Maengo maarufu kama S2kizzy au Zombie ni mtayarishaji muziki na mwandishi wa nyimbo nchini Tanzania ambaye ametangaza ujio wa albamu yake mpya.
Zombie anayefahamika kwa kutayarisha nyimbo kama “Amaboko” na “Tetema” za Rayvanny akimhusisha Diamond platnumz, amefichua jina la kazi hiyo inayotarajiwa ya sanaa ambalo ni “Virus”.
Anatarajiwa kuizindua rasmi Novemba 13, 2026 na katika tangazo hilo, S2kizzy ameonyesha dhamira ya kuendelea kupanua wigo wake katika tasnia ya muziki, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kufahamu aina ya kazi zitakazopatikana kwenye album hiyo.
Z2kizzy ambaye amejijengea jina kubwa kupitia utayarishaji wa nyimbo mbalimbali zilizofanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, sasa anajiandaa kuandika ukurasa mwingine wa safari yake ya kisanii kupitia mradi huo.
Jina la album hiyo, ‘VIRUS’, limeongeza hamasa na maswali miongoni mwa wadau wa burudani kuhusu ujumbe na ladha ya muziki atakayokuja nayo.
Hata hivyo, bado haijawekwa wazi orodha kamili ya nyimbo pamoja na wasanii watakaoshirikishwa katika album hiyo.