Tems ashinda tuzo ya Grammy

Alishinda tuzo hiyo kupitia wimbo wake 'Love me Jeje' katika kitengo cha cha tumbuizo bora la muziki wa Afrika.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa kike wa Nigeria Temilade Openiyi, maarufu kama Tems, amejishindia tuzo yake ya pili ya Grammy.

Mrembo huyo aliibuka mshindi katika kitengo cha tumbuizo bora la muziki wa Afrika au ukipenda ‘Best African Music Performance’.

Katika awamu ya 67 ya tuzo hizo za Grammy, Tems aliwashinda Burna Boy, Davido, Asake, Yemi Alade, Odas na Chris Brown kupitia kibao chake kiitwacho ‘Love Me Jeje’.

Katika hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo, tems alimshukuru Mungu kwa kumweka kwenye jukwaa hilo na kwa kumpa kundi bora analoshirikiana nalo.

Aliongeza kutangaza kwamba leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya mamake mzazi aliyeambatana naye wakati wa kupokea tuzo hiyo huku akimshukuru.

Hii sio tuzo ya kwanza ya Grammy kwa kidosho huyo mwenye sauti tamu kutoka Nigeria kwani katika awamu ya 65 ya tuzo hizo, alishinda tuzo katika kitengo cha tumbuizo la muziki bora wa kufokafoka wenye wimbo mtamu yaani ‘Best Melodic Rap Performance’ kupitia kibao kiitwacho ‘Wait For You’ ambapo yeye na Drake walishirikishwa na mwanamuziki Future.

Katika awamu ya mwaka huu, Tems alikuwa amepata uteuzi katika vitengo vinane.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *