Femi One amtangazia Hezeh Ndung’u kazi zake

Awali wengi walidhania kwamba wawili hao ni baba na mwana.

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii wa muziki wa mtindo wa Rap nchini kenya Wanjiku Kimani maarufu kama Femi One, amemtangazia mwanamuziki mwenza Hezeh Ndung’u kazi zake kupitia akaunti yake ya Instagram.

Femi alichapisha video fupi yenye picha yake ya pamoja na Hezeh na kuandika, “Ni Jumapili furahia muziki wa Hezeh Ndung’u, saidia biashara ya familia,” akimalizia na emoji ya kucheka.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2024, uvumi ulisambaa mitandaoni kwamba Hezeh Ndung’u ndiye baba mzazi wa mwanamuziki Femi One, baada ya picha hiyo ya pamoja kusambaa mitandaoni.

Wengi walishangaa uhusiano wa wawili hao ikitizamiwa kwamba Mzee Ndung’u wa dhehebu la Akorino huimba nyimbo za injili huku Femi akiimba nyimbo za dunia.

Lakini baadaye Femi alifafanua kwamba Hezeh sio babake mzazi bali ni mwanamuziki ambaye anamheshimu sana kwa kazi zake.

Katika mahojiano, Femi alishangaa jinsi uvumi huo uliundwa na kusambaa kwa kasi huku wengi wakidhania ni ukweli hata baada ya ufafanuzi.

Alisema babake mzazi alikuwa akiitwa Peter Kimani na aliaga dunia.

Share This Article